

**TAARIFA YA AJALI YA KAKA ANDREW SANGA**
Ndugu Wanajumuiya,
Kama ambavyo tumesikia kwenye mitandao asubuhi hii ya leo ndugu yetu Andrew Sanga (Drew) amepata ajali ya kupigwa risasi. Kesi bado iko mikononi mwa polisi na tutatoa taarifa rasmi ya tukio pindi tutakapopata habari kamili.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia Bw. Prosper Kiswaga hali ya Andrew siyo nzuri na kwasasa yupo ICU hospitali ya Memorial Hermann Southwest , 7600 Beechnut St, Houston, TX 77074
Kwa mujibu wa Bw. Kiswaga , madaktari wanashauri kusiwe na mkusanyiko mkubwa wa watu hospitalini hapo hadi hali ya ndugu yetu Andrew itakapotengamaa.
Mama mtoto wa Andrew , Bi. Emmy Matafu ( Mama Zoe ) yupo hapo hospitali kwenye chumba maalumu na tunaweza kwenda kumfariji na kumpa nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Ndugu Wanajumuiya, Andrew Sanga anahitaji maombi yetu katika kipindi hiki ili aweze kuvuka salama katika mtihani huu na hatimaye kuungana tena na familia yake
Kila mtu kwa imani yake tumuombee kaka Andrew.
Taarifa zaidi zitawajia kila zitakapopatikana
Ahsanteni
Cassius Pambamaji
Msemaji wa THC
Powered by #MaPROMO BLOG - A Division of J & P ENT - All Rights Reserved